Mpango Mkakati · Julai 2026 – Juni 2036
Miaka Kumi Yenye Mafanikio — Kwa Pamoja Tuujenge Ufalme wa Mungu
“Haya! Na tuondoke tukajenge.” Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema. Nehemia 2:18
Neno la Mchungaji Kiongozi
“Huu si waraka tu wa kimaandishi; ni maono tuliyobeba kutoka madhabahuni kwa ajili ya mustakabali wa kanisa letu na jamii inayotuzunguka hapa makao makuu ya nchi. Hakuna aliye mdogo, na hakuna wa kubaki nyuma.”
Mch. Joseph Stanley Masinga · Mchungaji Kiongozi
Nguzo Kuu
Nguzo Tano za Mkakati
- 1
Ukuaji wa Kiroho na Malezi
Lengo: Washirika wasiwe wasikilizaji tu bali wanafunzi wa kweli wa Kristo.
Mkakati: Makanisa ya nyumbani (Cell Ministry), semina za kila robo mwaka, madarasa ya waongofu wapya.
- 2
Uinjilisti na Upanuzi
Lengo: Kujenga kanisa la kudumu na kufungua matawi mapya.
Mkakati: Mkutano mkubwa wa Injili kila mwaka na matawi 5 nje ya Nzuguni ndani ya miaka 10.
- 3
Utawala na TEHAMA
Lengo: Mifumo imara ya uongozi na utendaji wa kisasa.
Mkakati: Mfumo wa kidijitali wa kanisa na mafunzo ya uongozi mara mbili kwa mwaka.
- 4
Fedha na Miundombinu
Lengo: Miradi ya kimkakati ya maendeleo na vitega uchumi.
Mkakati: Idara imara na miradi ya kiuchumi kama ukumbi wa sherehe au shule.
- 5
Huduma kwa Jamii
Lengo: Kuwafikia wahitaji katika jamii inayotuzunguka.
Mkakati: Mfuko wa wasiojiweza, yatima na wajane; kliniki za afya na sheria angalau mara moja kwa mwaka.
Utekelezaji
Awamu Tatu
Jul 2026 – Jun 2029
Awamu I: Kuweka Msingi
Jengo la kanisa, vyombo vya madhabahu na muziki, mifumo na TEHAMA.
Jul 2029 – Jun 2032
Awamu II: Mafanikio ya Kihuduma
Matawi mapya, uinjilisti na huduma ya Daycare.
Jul 2033 – Jun 2036
Awamu III: Kudumisha Mafanikio
Uwekezaji endelevu kwenye miradi na utulivu wa kanisa.
“Mimi ni mshirika wa Ebenezer Temple. Mpango huu ni dira yangu, maono haya ni wajibu wangu. Sitakuwa mtazamaji; mimi ni sehemu ya mafanikio haya.”
Changia Mpango Mkakati