Ebenezer TempleHema ya Sifa · Nzuguni ‘B’

Kuhusu Sisi

Hata Sasa Bwana Ametusaidia

“Ebenezer” – 1 Samweli 7:12

Historia Yetu

Ebenezer Temple, Nzuguni ‘B’

Ebenezer Temple ilianzishwa tarehe 29 Juni 2025 hapa Nzuguni ‘B’, Dodoma, kama tawi la Kanisa la Tabernacle of Praise Church (TOPC) – Hema ya Sifa. Lengo letu ni kuwa kitovu cha ibada halisi, mafundisho ya kweli ya Neno la Mungu, na mabadiliko ya kijamii katika makao makuu ya nchi yetu yanayokua kwa kasi.

Katika mwaka wetu wa kwanza Bwana ametusaidia – “Ebenezer”. Washirika wameongezeka kutoka 58 hadi 125, tumejenga jengo la muda la ibada, tumepata vyombo vya muziki na mfumo wa sauti, na idara za Wanawake, Wanaume, Vijana, Uimbaji na Kanisa la Watoto zimeimarika.

Dira

Kuwa na kanisa lenye nguvu za Mungu, linalogusa maisha ya watu kiroho, kiuchumi, na kuwa kitovu cha mabadiliko chanya mkoani Dodoma na Tanzania yote.

Utume

Kumfanya kila mtu kuwa mwanafunzi thabiti wa Yesu Kristo kupitia mahubiri ya Injili, mafundisho yenye uzima, malezi ya kiroho, na huduma za upendo na huruma kwa jamii.

Tamko la Imani

Tunachokiamini

Biblia

Biblia imevuviwa na Mungu, haina makosa, na ni Neno lenye mamlaka ya Mungu.

2 Tim 3:16; 1 Kor 2:13

Utatu Mtakatifu

Mungu mmoja wa milele katika nafsi tatu – Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Mt 28:19; 2 Kor 13:14

Yesu Kristo

Uungu wake, kuzaliwa na bikira, maisha yasiyo na dhambi, kifo cha msalaba, ufufuo wa mwili, kupaa kwake na kurudi kwake mara ya pili kwa utukufu.

1 Kor 15:1-4; Yoh 14:2-3

Wokovu kwa Neema

Wokovu ni kwa neema kupitia toba na imani katika kazi kamilifu ya msalaba wa Kalvari.

Efe 2:8-9; Ebr 9:12,22

Ubatizo wa Maji

Ubatizo wa maji mengi kwa kuzamishwa katika jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Mt 28:19; Mdo 19:1-6

Roho Mtakatifu

Huduma ya Roho Mtakatifu humwezesha mwamini kuishi maisha ya uchaji Mungu; kunena kwa lugha ni ishara ya awali ya kujazwa Roho.

Mdo 2:4

Muhtasari kutoka Katiba ya TOPC, Ibara ya 3.

Maadili Yetu

  • Utakatifu na Uaminifu

    Kuishi maisha yanayomtukuza Mungu sirini na dhahiri.

  • Upendo na Umoja

    Kujali wengine na kushirikiana kama mwili mmoja wa Kristo.

  • Ubora

    Kufanya kazi ya Mungu kwa moyo wa kujitolea.

  • Unyenyekevu na Utumishi

    Kuongoza kwa mfano wa Kristo kwa kuwatumikia wengine.

Idara za Kanisa

  • Idara ya Wanawake
  • Idara ya Wanaume
  • Idara ya Vijana
  • Idara ya Uimbaji (Kwaya)
  • Kanisa la Watoto (Sunday School)

Uongozi

Mchungaji na Wazee wa Kanisa

Mchungaji Kiongozi

Joseph Stanley Masinga

Mchungaji Kiongozi wa Ebenezer Temple, Nzuguni ‘B’ – Dodoma. Mwenye maono ya “Kwa Pamoja Tuujenge Ufalme wa Mungu”.