Tabernacle of Praise Church
Karibu Ebenezer Temple
“Hema ya Sifa” · Nzuguni ‘B’, Dodoma
Ebenezer Temple ni familia ya waamini wa Tabernacle of Praise Church (Hema ya Sifa) hapa Nzuguni ‘B’, Dodoma. Njoo uabudu pamoja nasi, ukue katika Neno, na uwe sehemu ya kazi ya Mungu katika jiji letu.
Karibu Nyumbani
Miaka Kumi Yenye Mafanikio — Kwa Pamoja Tuujenge Ufalme wa Mungu
“Haya! Na tuondoke tukajenge.” Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema.
— Nehemia 2:18
Dira
Kuwa na kanisa lenye nguvu za Mungu, linalogusa maisha ya watu kiroho, kiuchumi, na kuwa kitovu cha mabadiliko chanya mkoani Dodoma na Tanzania yote.
Utume
Kumfanya kila mtu kuwa mwanafunzi thabiti wa Yesu Kristo kupitia mahubiri ya Injili, mafundisho yenye uzima, malezi ya kiroho, na huduma za upendo na huruma kwa jamii.
Ukuaji kwa Neema ya Mungu
- Washirika
- 125+
- kutoka 58 mwaka wa kwanza
- Tulianza
- 2025
- 29 Juni
- Idara Hai
- 5
- Wanawake, Wanaume, Vijana…
- Matawi Lengwa
- 5
- ifikapo 2036
Ratiba na Mahali
Ratiba ya Wiki
Jumapili
Ibada Kuu ya Jumapili
09:00 – 12:30
Jumapili
Kanisa la Watoto (Sunday School)
09:00 – 12:00
Jumatano
Maombi na Mafundisho ya Katikati ya Juma
17:30 – 19:00
Ijumaa
Ushirika wa Vijana
17:30 – 19:00
Jumamosi
Ushirika wa Wanawake / Mazoezi ya Kwaya
15:00 – 17:00
Ushirika
Matukio Yanayokuja
Hakuna matukio yaliyopangwa kwa sasa. Rudi tena hivi karibuni.
Matangazo
Hakuna matangazo mapya.
Mahubiri
Mahubiri ya Hivi Karibuni
Mahubiri yatawekwa hapa hivi karibuni.
Mpango Mkakati 2026 – 2036
Nguzo Tano za Mpango Mkakati
- 01
Ukuaji wa Kiroho na Malezi
Washirika wasiwe wasikilizaji tu bali wanafunzi wa kweli wa Kristo.
- 02
Uinjilisti na Upanuzi
Kujenga kanisa la kudumu na kufungua matawi mapya.
- 03
Utawala na TEHAMA
Mifumo imara ya uongozi na utendaji wa kisasa.
- 04
Fedha na Miundombinu
Miradi ya kimkakati ya maendeleo na vitega uchumi.
- 05
Huduma kwa Jamii
Kuwafikia wahitaji katika jamii inayotuzunguka.
Toa Sadaka
Toa Zaka na Sadaka kwa Simu Yako
M-Pesa · Mixx by Yas · Airtel Money · HaloPesa — Zaka, Sadaka, Ujenzi na Mpango Mkakati wa Miaka Kumi.
